Jerzy Buzek amewaambia waandishi habari kwamba demokrasia haifanyi mabadiliko ya aina yoyote katika mafundisho ya dini kwa sharti kwamba serikali ijitawale na kuendesha shughuli zake za kisiasa kwa uhuru kamili. ‘Nina imani kwamba demokrasia inayosimama juu ya misingi ya Uislamu itakuwa na mafanikio’ amesisitiza Mkuu wa Bunge la Ulaya.
Amesema Umoja wa Ulaya unaunga mkono matokeo ya uchaguzi wa Tunisia na chama cha an Nahdha kilichopata ushindi katika uchaguzi huo kwa sababu ulifanyika kwa uwazi na uhuru kamili.
Jerzy Buzek amesema kuwa tokea sasa Umoja wa Ulaya utatayarisha mazingira mazuri ya kutolewa viza kwa wanafunzi wa Tunisia na nchi za bara hilo zitadumisha shughuli zao za kibiashara nchini Tunisia.
891238