IQNA

Nafasi muhimu ya Lebanon katika maonyesho ya magazeti ya kimataifa

13:00 - November 03, 2011
Habari ID: 2216866
Mwaka huu Lebanon imekuwa na nafasi muhimu katika duru ya 18 ya maonyesho ya magazeti na mashirika ya habari ya kimataifa ambayo yalimalizika hivi karibuni mjini Tehran.
Nchi hiyo ilishiriki kwenye maonyesho hayo kwa kuonyesha shughuli za magazeti yake kadhaa ambayo ni as-Swafir, at-Thabaat, al-Akhbar na jarida la al-Wahda.
Akizungumzia shughuli za magazeti na majarida hayo, Zahir Badrudeen, msimamizi wa kibanda cha Lebanon katika maonyesha hayo amesema kwa ufupi kwamba magazeti na majarida hayo hujishughulisha na kuakisi maudhui mbalimbali ya kisiasa, kiutamaduni, kiuchumi na kijamii yanayotokea nchini humo.
Badrudeen ambaye ni mhariri mkuu wa gazeti la Wakalatul Akhbar Lubnan amefafanua shughuli za gazeti hilo na kusema kuwa huakisi habari zote zinazohusiana na masuala ya kisiasa, kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na lugha ya Kiarabu kitaifa.
Amesema gazeti hilo lilianzishwa mwaka 1959 na Abbas Badrudeen, mwandishi wa Lebanon ambaye alitekwa nyara na utawala wa dikteta Mummar Gaddafi akiwa na Imam Musa Sadr mwanazuoni na mwanafikra mashuhuri wa Lebanon. Amesema licha ya kutoa kipaumbele kwa habari za ndani ya Lebanon, gazeti hilo pia huakisi matukio muhimu ya kimataifa. 891615
captcha