Kwa mujibu wa tovuti ya walf, kamati iliyotajwa ambayo iiko chini ya Baraza la Waislamu wa Ufaransa CFCM, imesema kuwa katika kipindi cha miezi tisa ya mwanzo ya mwaka huu vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu Ufaransa vimeongezeka kwa asilimia 22 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Abdallah Dhakiri amesema kwamba kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo ilitolewa kwenye nyaraka za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa, kesi 115 za malalamiko ya Waislamu ikiwa ni pamoja na chuki, ubaguzi, kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu pamoja na wanawake wanaovaa hijabu na uchomaji moto Qur'ani zimeripotiwa na Waislamu katika mahakama tofauti za Ufaransa.
Amesema katika sehemu nyingine ya matamshi yake kwamba vitendo vya ubaguzi pekee dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo vimeongezeka kwa asilimia 50 mwaka huu ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Amesema kuwa idadi hiyo imeongezeka kwa kiwango hicho kutokana na kuwa wagombea katika chaguzi mbalimbali za nchi hiyo wamekuwa wakiwatumia Waislamu kama vyombo tu vya kufikia maslahi yao ya kisiasa. 892845