Shirika la Habari la Reuters limeandika kwamba licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na utawala wa Kiwahabi wa Saudia wa kuwazuia mahujaji kupanda Mlima wa Nur na Pango la Hira lakini mahujai wengi hupuuza suala hilo na kwenda kwa wingi kwenye pango hilo lililoko kwenye Mlima Nur ambapo ndipo wahyi wa kwanza ulimteremkia Bwana Mtume (saw).
Shirika hilo la habari limeendelea kusema kuwa licha ya umuhimu mkubwa wa eneo hilo katika historia ya Kiislamu, lakini utawala wa Saudia huwazuia mahujaji kwenda huko ili wasifanye mambo yanayokwenda kinyume na mafundisho ya uongo na batili ya Mawahabi.
Ripoti hiyo inaendelea kusema kuwa Mawahabi wameweka askari wengi katika eneo hilo wanaowazuia mahujaji kukaribia maeneo hayo matakatifu. Wameandika mabango na matangazo yanayowatahadharisha mahujai wanaokwenda huko kuyazuru kwamba ziara na kuswali katika maeneo hayo si sehemu ya hija na kwamba ni mambo yanayokwenda kinyume na mafundisho ya Kiislamu kwa mtazamo wa Mawahabi.
Ilani zilizoandikwa kwenye mabango hayo zinadai kwamba kuswali kwenye maeneo kama hayo huenda kukawa ni shirki. 892876