IQNA

Mahujaji milioni tatu wasimama Arafa

18:37 - November 05, 2011
Habari ID: 2217923
Waislamu zaidi ya milioni 3 leo Jumamosi wametekeleza ibada muhimu ya kusimama kwenye mlima wa Arafa ikiwa ni sehemu muhimu ya amali za hija kwa mahujaji wanaozuru Nyumba ya Mwenyezi Mungu al-Kaaba.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Palestina Maa, mahujaji hao walianza kumiminika katika eneo hilo takatifu baada ya kuswali swala ya Ijumaa hapo jana katika Msikiti wa Haram.
Mahujai wengine hiyo jana walielekea Mina kwa ajili ya kutekeleza marasimu ya tarwiya kabla ya kuelekea leo katika jangwa la Arafa ili kunong'ona ma Mola wao kupitia dua muhimu zinazosomwa huko.
Kwa mujibu wa takwimu rasmi karibu Waislamu milioni tatu wanafanya hija mwaka huu ambapo milioni moja na laki nane wanatoka nje ya Saudia na waliosalia wanatoka nchini humo na nchi nyingine za Ghuba ya Uajemi.
Siku ya tarehe 8 Dhulhija imetajwa kuwa ni siku ya tarwiya kwa sababu hakuna maji katika maeneo ya jangwani ya Mina na Arafa na kwa hivyo mahujaji wanaoelekea katika maeneo hayo wanapasa kujibebea maji na kwenda nayo huko.
Siku hiyo ni moja ya siku muhimu za Dhulhija na kwa mujibu wa riwaya kutoka kwa Imam Swadiq (as) kufunga katika siku hii humkidhia mja kafara yake ya miaka 60. 892941
captcha