Mwanamfalme Nayif bin Abdul Aziz amesema kuwa idadi ya mahujaji kutoka nje ya nchi waliokwenda Makka kwa ajili ya ibada ya hija mwaka huu imepita milioni moja na laki nane.
Ameongeza kuwa idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia 1.5 ikilinganishwa na mwaka jana. Amesema kuwa idadi kubwa ya mahujaji wa kigeni katika ibada ya hija ya mwaka huu haijawahi kushuhudiwa nchini Saudia.
Inakadiriwa kuwa watu karibu milioni tatu wanatekeleza ibada ya hija mwaka huu nchini Saudia laki saba kati yao wakiwa wenyeji wa nchi hiyo. 893452