IQNA

Hali ya kiutamaduni na kijamii ya Waislamu wa kaskazini mwa Afrika kuchunguzwa

19:58 - November 06, 2011
Habari ID: 2218543
Kikao cha kuchunguza hali ya kiutamaduni na kijamii ya Waislamu wa kaskazini mwa Afrika kimepangwa kufanyika hivi karibuni katika Kituo cha Utamaduni, Sanaa na Mawasiliano cha Wizara ya Mwongozo wa Kiislamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kikao hicho kimepangwa kufanyika siku ya Jumatano tarehe 9 Novemba. Katika kikao hicho Ahmad Ali Qani', mwanachama wa jopo la kielimu katika Chuo Kikuu cha Imam Swadiq (as) atazungumzia matatizo yanayowakumba Waislamu wa Afrika katika nyanja za utamaduni, dini, uchumi na masuala ya kijamii.
Hali ya kawaida ya Waislamu wa magharibi mwa Afrika na misaada ya nchi nyingine za dunia kwa nchi za Afrika ni masuala mengine yatakayochunguzwa kwenye kikao hicho cha kitaalamu.
Waandaaji wa kikao hicho wanasema kuwa kitaanza saa nne na kuendelea hadi saa sita ambapo wanachuo, watafiti na wahadhiri wengi wamealikwa kuhudhuria kikao hicho. 894141
captcha