Kituo cha habari cha CPI kimeripoti kuwa kwa mujibu wa mpango huo utawala haramu wa Israel utajenga nyumba 60,718 za walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu za Quds Tukufu katika kipindi cha miaka 20 ijayo.
Magazeti ya utawala haramu wa Israel yameandika kuwa ramani ya ujenzi wa nyumba 13,500 imekwishatayarishwa na ujenzi wake utaanza miaka kadhaa ijayo.
Utawala huo haramu pia unapanga kujenga nyumba 10934 katika eneo la Salwan lililoko kusini mwa Msikiti wa al Aqsa. 894909