IQNA

OIC yalaani mashambulio ya kigaidi Nigeria

16:39 - November 08, 2011
Habari ID: 2219275
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC ametoa taarifa akilaani vikali mashambulio ya kigaidi ya hivi karibuni nchini Nigeraia.
Katika taarifa hiyo, Ekmeleddin Ihsanoglu amelaani mashambulio hayo dhidi ya misikiti na makanisa pamoja na kuuawa watu wasio na hatia na kusema kuwa vitendo hivyo vya jinai vinakinzana na thamani zote za kiutu na kidini na kuongeza kuwa watekelezaji wa vitendo hivyo hawaheshimu hata kidogo roho za watu.
Amesema, kama kawaida OIC inalaani vikali vitendo vya ugaidi wa aina yoyote na ameyataka makundi yote ya kisiasa na kijamii ya Nigeria kuheshimu misingi ya Uislamu na kujiepusha na vitendo vya utumiaji mabavu.
Wakati huohuo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ametoa mkono wa pole kwa familia za wahanga wa matukio hayo ya kigaidi na kuelezea matumaini yake kwamba anataraji wahusika wa vitendo hivyo watatiwa nguvuni na kuhukumiwa na serikali haraka iwezekanavyo.
Mamia ya watu waliuawa na kujeruhiwa katika matukio hayo ya kigaidi ambayo yalitekelezwa hivi karibuni dhidi ya misikiti, makanisa na vituo vya polisi katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria. 894661
captcha