Akizungumza hivi karibuni mbele ya Taassi ya Kitaifa ya Demokrasia nchini Marekani NDI, Waziri Hillary Clinton amedai kwamba serikali ya Washington iko tayari kushirikiana na Waislamu walioshinda uchaguzi wa hivi karibuni nchini Tunisia.
Katika kudumisha siasa za hadaa za serikali ya Washington, Clinton amesema kuwa fikra za makundi yote ya Kiislamu hazifanani na amekitaka chama cha an-Nahdha kilichoshinda uchaguzi kushirikiana na watu wanaopinga utawala wa kidini nchini humo na kwamba serikali ya Marekani itashirikiana na chama hicho iwapo kitatekeleza takwa hilo la Washington.
Huku akisema kuwa chama cha an-Nahdha kimeahidi kuheshimu uhuru wa kidini na haki za binadamu zikiwemo za wanawake, Clinton amedai kwamba kwa kawaida makundi ya Kiislamu duniani hushindwa kutekeleza vyema demokrasia.
Akiwalenga Waislamu kwa kejeli, amesema vyama vya Kiislamu vinapasa kuheshimu demokrasia, kujiepusha na vitendo vya mabavu, kuheshimu sheria, uhuru, haki za binadamu na kujiepusha kuchochea hisia za kidini. 894994