IQNA

Mahujaji wa Bahrain waandamana Makka dhidi ya utawala wa Aal Khalifa

17:58 - November 09, 2011
Habari ID: 2220010
Mahujaji wa Kibahrain jana Jumanne walifanya maandamano katika mji mtakatifu wa Makka wakipiga nara dhidi ya utawala wa Aal Khalifa na wamelaani vikali ukandamizaji unaofanywa na serikali ya Manama nchini Bahrain.
Shirika la habari la Nun limeripoti kuwa katika maandamano hayo mahujaji wa Bahrain wamesisitiza juu ya udharura wa kupinduliwa serikali ya Aal Khalifa na kutoa wito wa kudumishwa maandamano hadi utawala huo utakapong'olewa madarakani.
Wapinzani wa utawala wa Bahrain wanaendelea kufanya maandamano nchini humo na licha ya ukandamizaji mkubwa unaofanywa na jeshi la nchi hiyo likishirikiana na askari wa Saudi Arabia lakini wangali wanasisitiza juu ya kutimizwa matakwa yao.
Hadi sasa watu 45 wameuawa shahidi na mamia ya wengine kujeruhiwa katika harakati ya mapinduzi ya watu wa Bahrain. 895418


captcha