IQNA

Utawala wa Bahrain wabana matumizi ya intaneti nchini

21:58 - November 10, 2011
Habari ID: 2220145
Taasisi ya Freedom House ya Marekani imesema kwamba utawala wa Aal Khalifa nchini Bahrain umebana sana shughuli za mtandao za wanaharakati wa haki za binadamu nchini humo.
Ripoti ya tarehe 8 Novemba ya taasisi hiyo, inasema kuwa utawala huo umekuwa ukikandamiza wanaharakati hao pamoja na jamii ya madaktari wa nchi hiyo kufuatia matukio ya kisiasa yanayoendelea nchini humo. Imesema kufuatia mashinikizo hayo ya kidhulma dhidi ya wanaharakati wa haki za binadamu tayari wanaharakati mashuhuri 31 wametiwa nguvuni na mmoja wao ameripotiwa kuuawa akiwa mikononi mwa askari usalama wa utawala huo.
Freedon House imesema kuwa wananchi wa Bahrain kama walivyo wananchi wa nchi nyingine wana haki ya kupigania mabadiliko ya kisiasa na kidemokrasia nchini kwao. Imesema Wabahrain wamekuwa wakipigania haki zao za kimsingi zikiwemo za uadilifu wa kijamii na kuheshimiwa sheria, jambo ambalo limekuwa likipingwa na utawala wa Aal Khalifa na kuwakandamiza wateteaji wa haki hizo ilihali ulimwengu umekaa kimya bila kuchukua hatua zozote za kuwatetea.
Tasisi hiyo ya kutetea uhuru duniani iliyo na makao yake nchini Marekani imeendelea kusema kuwa, Wabahrain kama walivyo wananchi wa nchi nyingine za Kiarabu, walitarajia kushuhudia mabadiliko ya kidemokrasia katika nchi yao kutokana na wimbi la mabadiliko ya kisiasa katika nchi kadhaa za Kiarabu lakini kwa bahati mbaya hali ya mambo imewaendelea mrama na kuwafanya wanamapinduzi wa nchi hiyo kuwa wahanga wa ukandamizaji na dhulma ya utawala wa Aal Khalifa.
Taasisi ya Freedom House ni taasisi iliyoasisiwa mwaka 1941 kwa lengo la kusaidia kueneza demokrasia, kuunga mkono uhuru wa kisiasa na kiraia na kutetea haki za binadamu katika pambe mbalimbali za dunia.
Tokea mwaka 1972 taasisi hiyo imekuwa ikitoa ripoti kila mwaka kuhusiana na hali ya kidemokrasia, haki za binadamu na kisiasa katika nchi tofauti. 895919
captcha