IQNA

Sheikh Seddiqi:

Uchokozi wowote dhidi ya Iran utajibiwa kwa nguvu

16:21 - November 12, 2011
Habari ID: 2221103
Khatibu wa sala ya Ijumaa iliyosaliwa mjini Tehran amezitahadharisha nchi za Magharibi kwamba uchokozi wowote zitakaoanzisha dhidi ya ardhi ya Iran utajibiwa kwa nguvu.
Hujjatul Islam Kazem Seddiqi amesema kuwa, vikosi vya jeshi la ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran viko tayari kujibu shambulio lolote litakaloanzishwa na maadui dhidi ya ardhi ya nchi hii.
Hujjatul Islam Seddiqi amesema kuwa, Marekani, Uingereza na Ufaransa ni madola dhaifu na hafifu ambayo katu hayawezi kupata ushindi hata siku moja na kwamba, ushindi daima huwaendea watu wenye nyoyo za imani na uchaji-Mungu.
Khatibu wa sala ya Ijumaa mjini Tehran amezungumzia pia wimbi la mwamko wa Kiislamu ambalo limebadilisha kikamilifu taswira ya historia na kuyaweka mataifa ya kibeberu katika hali ya kiwewe. Amesisitiza kuwa, wimbi hilo la mwamko katika Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika linapaswa kutoa funzo kwa watawala wa ulimwengu wa Kiislamu kwamba, wananchi wao hawataki chochote ghairi ya sheria za Kiislamu zilizojaa umaanawi, haki na zenye kulinda maslahi ya watu wote.
Khatibu wa sala ya Ijumaa mjini Tehran ameongeza kuwa, mataifa ya kibeberu hayatapata usingizi na kwamba daima yanakesha yakibuni maovu ya kuielekezea Jamhuri ya Kiislamu ili kujaribu kuficha fedheha ya kufeli kwa sera zao za kiliberali, kibepari na kibeberu.
895643
captcha