Kitabu hicho kimechapishwa nchini Ujerumani baada ya gazeti la Charlie Hebdo la Ufaransa kuchapisha picha zinazomkebehi na kumvunjia heshima Mtume wa Mwenyezi Mungu Muhammad (saw).
Kitabu hicho kimechapishwa kwa njia isiyokuwa rasmi kikimvunjia heshima Mtume na kutaja vita vya Waislamu dhidi ya washirikina na makafiri wa zama za awali za Uislamu kuwa ni jinai!
Baada ya kugundua kwamba kitabu hicho kinasambazwa nyumba kwa nyumba nchini Ujerumani, wiki iliyopita Waislamu wa nchi hiyo walikusanyika katika miji mbalimbali wakiitaka serikali kusimamisha uchapishaji wa kitabu hicho.
Vyombo vya habari vya Ujerumani vimetangaza kuwa mahakama za nchi hiyo zinafuatilia kadhia hiyo ili kumtambua mwandishi na mahala kinakochapishwa. 896472