Maonyesho hayo yanafanyika kwa lengo la kuarifisha maisha na utamaduni wa Waislamu na ada za Kiislamu.
Katika maonyesho hayo kuna kazi 250 za sanaa ya Kiislamu zinazoakisi aina mbalimbali ya maisha na ada za Waislamu katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu wa Kiislamu.
Idara ya Jumba la Makumbusho la Berlin imetangaza kuwa maonyesho hayo yanaakisi irfani, usufi na misingi ya dini ya Kiislamu na vilevile harakati za kidini katika maisha ya kila siku ya Waislamu wa nchi za kaskazini mwa Afrika hadi Asia ya Kati.
Imesema kuwa kazi zinazoonyeshwa katika maonyesho hayo zinabainisha sanaa ya usanifu majengo katika ulimwengu wa Kiislamu na mtazamo wa Uislamu kuhusu umuhimu wa kuimarisha nafasi ya mwanamke katika familia na vilevile nafasi ya mwanaume katika maisha ya kijamii. 897426