Kwa mujibu wa shirika la RiaNovosti, msahafu huu una ukubwa wa sentimita 150x200, kurasa 632 na uzito wa kilo 800. Jalada la msahafu huu limetengenezwa kwa malakati na mawe yenye thamani na kupambwa kwa dhahabu na shaba.
Msahafu huu utawekwa katika ukumbi wa Msikiti wa Qolsharif na ifikapo Juni 2012 utapelekwa katika eneo la Bolgary huko Tatarstan na kuwekwa katika jiwe la ukumbusho ambalo liliwekwa kwa mnasaba wa Uislamu kuwa dini rasmi ya Volga Bulgaria mwaka 922.
899144