Gazeti la Nation limeripoti kuwa ripoti ya FBI inaonyesha kwamba, kwa mfano tu jinai na uhalifu unaosababishwa na chuki dhidi ya Waislamu umeongezeka kutoka kesi 107 mwaka 2009 hadi 160 mwaka 2010.
Pamoja na hayo takwimu hizo haziakisi ukweli wa mambo kuhusu ukatili na jinai zinazofanywa dhidi ya Waislamu nchini Marekani, kwani polisi ya FBI huwa hairipoti mambo yote yanayotokea.
Wataalamu wa mambo wanasema kuwa sehemu moja ya ongezeko la ukatili na jinai dhidi ya Waislamu ni matokeo ya hotuba na matamshi yanayotolewa na wanasiasa na makundi yenye misimamo mikali ya Marekani dhidi ya Uislamu likiwemo kundi la "Stop Islamization of America." 899464