IQNA

Hizbullah yakanusha madai ya utawala wa Bahrain

19:21 - November 16, 2011
Habari ID: 2223556
Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imekanusha tuhuma zilizotolewa na utawala wa Aal Khalifa nchini Bahrain uliodai kuwa umelitia nguvuni kundi la kigaidi lenye uhusiano na Hizbullah.
Harakati hiyo imesema madai hayo hayana msingi na yametolewa kwa lengo la kufunika ukweli wa mambo kuhusu mapinduzi ya amani ya wananchi wa Bahrain dhidi ya utawala wa nchi hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Hizbullah imesema kuwa madai ya utawala wa Aal Khalifa hayana msingi wowote na haijulikani kama watu wanaodaiwa kutiwa mbaroni walikuwa wanachama wa kundi la kigaidi au ni njama ya utawala wa Manama ya kutaka kudumisha utawala wao nchini Bahrain.
Taarifa hiyo imesema tuhuma zinazoihusisha Hizbullah na kundi linalodaiwa kuwa ni la kigaidi hazina ukweli wowote.
Hizbullah imesema madai hayo hayatadhoofisha mapambano ya wananchi wanaokandamizwa wa Bahrain ya kupigania haki zao za kisheria hadi watakapofikia malengo yao. 899234
captcha