IQNA

Majaji wa Mashindano ya Qur’ani Saudia waarifishwa

23:18 - November 17, 2011
Habari ID: 2223752
Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kidini ya Saudi Arabia imetangaza majini ya majaji wa Mashindano ya 33 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu yatakayofanyika nchini humo.
Kwa mujibu wa gazeti la Sabq, imearifiwa kuwa mashindano hayo yatasimamiwa na majaji wanne kutoka Saudia na sita kutoka nchi nyingine za Kiislamu.
Salman Ibn Mohammad Al Amri Mkuu wa Kamati ya Uhusiano wa Umma katika mashindano hayo amesema majaji Wasaudi katika mashindano hayo ni pamoja na Ibrahim ibn Sa’eed Aldsari, Emad ibn Zahir Hafez, Sheikh Sa’ud ibn Abdulaziz Alghanim na Salem Mahmoud Mahmoud Al-Shanqiti.
Majaji wa kimataifa katika mashindano hayo ni Ahmad Issa Hassan Al-Ma’sarawi kutoka Misri, Sheikh Samih Ahmad kutoka Jordan, Sheikh Mohammad Al-Mokhtar Al-Qasem Mohammad Al-Amin kutoka Mauritania, Sheikh Abdul Malek Abd Manaf Taher Lazem kutoka Malaysia, Taher Mohammad Rasul Hakim kutoka Pakistan na Shiekh Sadeq Sediq Zawiyah kutoka Nigeria .
Mashindano hayo yatafanyika katika mji mtakatifu wa Makka kuanzia 23-30 mwezi ujao wa Muharram. Kuna washiriki 161 kutoka nchi 53 duniani ambao watashiriki katika mashindano hayo ya qiraa na hifdhi ya Qur’ani Tukufu.
898584
captcha