IQNA

Saiful Islam Gaddafi atiwa nguvuni

16:08 - November 19, 2011
Habari ID: 2224791
Saiful Islam Gaddafi mwana wa dikteta aliyeuawa wa Libya Muammar Gaddafi, ametiwa nguvuni leo Jumamosi.
Waziri wa Sheria na Haki za Binadamu wa Libya Muhammad al Alaqi ametangaza kuwa Saiful Islam ametiwa nguvu huko kusini mwa Libya.
Vyombo vya habari vya Libya vimetangaza kuwa baada ya kutiwa nguvuni, Saiful Islam amesafirishwa kwa ndege ya helikopta na kupelekwa katika mji wa Zantan huko kaskazini mwa Libya.
Saiful Islam Gaddafi anasakwa pia na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa tuhuma za kutenda jinai dhidi ya binadamu. 900974
captcha