IQNA

Vikao vya Miujiza ya Qur’ani vyafanyika Iran

14:37 - November 20, 2011
Habari ID: 2225088
Taasisi ya Miujiza ya Qur’ani Tukufu ya Iran imeandaa vikao viwili ambavyo vimejadili miujiza ya Qur’ani Tukufu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, vikao hivyo vimejadili ‘Embriolojia katika Qur’ani’ na ‘Uundwaji Mvua na Mvua ya Mawe’.
Taasisi hiyo imesema itaandaa vikao vingine kujadili miujiza katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu.
Maudhui ya kila kikao hujadiliwa mapema na watafiti bingwa katika taalum husika ili kuandaa mijadala ya kitaalamu kuhusu miujiza ya Qur’ani.
Qur’ani Tukufu ina maneno ambayo yanathibitisha ni muujiza ya Mwenyezi Mungu. Qur’ani Tukufu ambayo aliteremshiwa Mtume Muhammad SAW zaidi ya karne 14 zilizopita, ina mifano mingi kuhusu maumbile ya mwanadamu ambayo wanasayansi wa karne za 20 na 21 wameanza kugundua.
Hadi sasa wataalamu wameweza kugundua machache tu kuhusu miujiza ya kisayansi ya Qur’ani Tukufu.
900495
captcha