IQNA

Maonyesho ya Qur'ani na vitabu vya vitabu vya Kiislamu yafanyika India

18:00 - November 20, 2011
Habari ID: 2225576
Maonyesho ya Qur'ani na vitabu vya Kiislamu yalimalizika jana katika jimbo la Bihar nchini India.
Maonyesho hayo ambayo yalifanyika kwa lengo la kuarifisha mafundisho ya Kiislamu kwa wasiokuwa Waislamu yalikuwa na tarjumi za Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kihindi na vitabu mbalimbali kuhusu Uislamu na Waislamu.
Msimamizi wa chumba cha taasisi ya uchapishaji ya Nour Anwar Rashid ya New Delhi amesema kuwa watu waliotembelea maonyesho hayo wamevutiwa mno na vitabu hususan tarjumi ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kihindi ambayo amesisitiza kuwa ni moja ya vitabu vilivyouzwa kwa wingi katika maonyesho hayo.
Amesema kuwa uzoefu wake wa miaka mingi katika kazi hiyo unaonyesha kuwa watu wasiokuwa Waislamu wanavutiwa mno na kununua tarjumi ya Qur'ani Tukufu na vitabu vya Kiislamu kwa lugha ya Kihindi. 901523



captcha