Uteuzi huo umefanyika katika mkutano wa kimataifa wa Turathi za Miaka 1000 za Najaf.
Mhariri Mkuu wa jarida la kila wiki la Asala la Iraq Ahmad Abdul Jabbar ameiambia IQNA kwamba mkutano wa Turathi za Miaka 1000 za Mji Mtakatifu wa Najaf umeuteuwa mji huo kuwa mji mkuu wa mazungumzo ya dini na staarabu mbalimbali mwaka 2014 na kwamba kazi hiyo imefanywa na jumuiya za Kiarabu na Kiislamu.
Ameongeza kuwa mkutano huo pia imepanga kuitisha kongamano la kimataifa la mazungumzo ya dini na staarabu mbalimbali mapema mwaka ujao mjini Beirut.
Ahmad Abdul Jabbar amesema kongamano hilo la kimataifa litahudhuriwa na makasisi wa Kikatoliki na maulamaa wa dini na madhehebu mbalimbali. 902433