Sheikh Ahmad al Tayyib ameutahadharisha utawala ghasibu wa Israel kuhusu taathira mbaya za njama hizo.
Amesema vitendo hivyo vitakuwa na taathira mbaya na hatari sana kwa eneo la Mashariki ya Kati na dunia nzima na kutishia usalama wa kimataifa. Amesisitiza kuwa kuyafanya maeneo ya Quds Tukufu kuwa ya Kiyahudi na kuharibu maeneo hayo matakatifu ni mshtari mwekundu ambao haupaswi kuvukwa.
Sheikh Tayyib amesema Quds kwa Waislamu ni ardhi ya Kiislamu inayokaliwa kwa mabavu na si kadhia ya Wapalestina pekee au ya Kiarabu, bali ni suala linalohusiana na itikadi za Kiislamu.
Amesisitiza kuwa Waislamu kote duniani wanapinga vitendo vya kuifanya Quds kuwa mali ya Wayahudi na kwamba vitendo hivyo vinakwenda kinyume na sheria za kimataifa. 902530