Huduma ya Kireno imezinduliwa Jumatatu Novemba 21 katika sherehe zilizofanyika katika makao makuu ya IQNA mjini Tehran.
Mkuu wa Taasisi ya Jihadi ya Vyuo Vikuu nchini Iran Mohammad Hussein Yadegari na Mkuu wa Tume ya Qur’ani katika Bunge la Iran Bi Laleh Iftikhari ni kati ya maafisa wa ngazi za juu walioshiriki katika hafla hiyo.
Shirika la Habari la Qur'an la Iran IQNA ndilo la kwanza na la pekee ambalo linashughulikia kwa njia maalumu habari za Qur'ani katika ulimwengu wa Kiislamu. Juhudi zetu daima zimekuwa ni kusambaza habari na ripoti za Iran na ulimwengu mzima kwa ujumla kuhusu masuala yanayohusiana na Qur'ani Tukufu pamoja na habari za kisiasa, kitamaduni, kisanaa, kiuchumi, kijamii vijana na watoto pamoja na kuzitathmini kwa mtazamo wa Qur'ani Tukufu.
Shirika hili lina matawi katika maeneo mengi ya dunia kama vile bara Afrika, Asia na Ulaya.
902926