IQNA

‘Ijumaa ya Kuiokoa al Aqsa’

16:31 - November 26, 2011
Habari ID: 2228497
Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu imeitaja Ijumaa ya Novemba 25 kuwa Siku ya Kuuokoa Msikiti wa Al Aqsa.
Kwa mujibu wa gazeti la Ash Sharq la Qatar, wito huo ulitolewa katika kipindi hiki ambacho Utawala wa Kizayuni wa Israel umekithirisha njama zake za Kuuyahudisha mji wa Quds (Jerusalem) na kuuharibu Msikiti wa Al Aqsa.
Taarifa ya jumuiya hiyo imesema Ijumaa hii imetajwa kuwa ‘Siku ya Kuuokoa Msikiti wa Al Aqsa’ ili kuuhami mji mtakatifu wa Quds na kuzuia njama za Wazayuni za kuubomoa Msikiti wa Al Aqsa.
Taarifa hiyo imetiwa saini na Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu Sheikh Yusuf Qaradawi na naibu wake Ali Al Qara.
Taarifa hiyo imesema jumuiya hiyo inaunga mkono juhudi za nchi za Kiislamu na Kiarabu za kukomboa Quds. Jumuiya hiyo pia imetoa wito kwa Waislamu kote duniani kuunga mkono harakati za mapambano ya Palestina, kubatilishwa mikataba yote eti ya amani na Wazayuni na kufukuzwa mabalozi wa utawala wa Kizayuni katika nchi za Kiarabu na Kiislamu.
904815

captcha