IQNA

Sayyid Nasrullah kuzungumza leo

16:49 - November 26, 2011
Habari ID: 2229190
Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon anatarajiwa kutoa hotuba muhimu hii leo Jumamosi kwa mnasaba wa kuanza mwezi wa majonzi na huzuni wa Muharram, huzini inayotokana na mauaji ya kinyama yaliyofanywa na Yazid bin Muawiya dhidi ya Imam Hussein (as) na wafuasi wake wachache watiifu.
Imam Hussein (as) ni mjuu wa Mtume Mtukufu (saw). Kwa mujibu wa tovuti ya elnashra, Sayyid Hassan Nasrullah atazungumza katika ukumbi wa Sayyid as-Shuhadaa ulioko kusini mwa mji mkuu Beirut kwa njia ya Video- Conference.
Vyombo vya kuaminika katika harakati ya Hizbullah vimesema kwamba Sayyid Nasrullah atazungumzia masuala mbalimbali ya kisiasa yanayohusiana na matukio ya kieneo na kimataifa.
Kwa mujibu wa ripoti zilizotufikia, harakati ya Hizbullah pia imepanga kufanya marasimu maalumu ya maombolezo ya kifo cha Imam Hussein (as) na wafuasi wake watiifu katika ukumbi uliotajwa ambapo Sayyid Hassan Nasrullah pia amepangiwa kuzungumza mara tano katika siku tofauti kuhusiana na maombolezo hayo. 905096
captcha