IQNA

Maombolezo ya Muharram Nigeria

15:25 - November 27, 2011
Habari ID: 2229869
Maombolezo ya kila mwaka ya Muharram yameanza Jumapili leo huko kaskazini mwa Nigeria.
Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaki ametangaza kuwa majlis za Muharram na maombolezo ya kukumbuka tukio la kuuawa shahidi mjukuu wa Bwana Mtume (saw) Imam Hussein (as) na wafuasi wake huko Karbala yanaanza leo Jumapili na ametoa wito kwa Waislamu kujitokeza kwa wingi katika majlisi hizo.
Majlisi hizo za maomolezo zitafanyika katika maeneo mbalimbali ya Kaskazini mwa Nigeria ikiwa ni pamoja katika Husseiniya ya Baqiyatullah katika jimbo la Zaria.
905426
captcha