IQNA

Onyo la Jumuiya ya Kiarabu kuhusu kikao cha Quds Tukufu

16:56 - November 27, 2011
Habari ID: 2229954
Kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kimeonya dhidi ya kufanyika kikao cha kwanza cha Shirika la Afya Duniani WHO cha eneo la bara Ulaya huko Quds Tukufu.
Kikao hicho kinatazamiwa kufanyika tarehe 28 Novemba. Kikao hicho cha Mawaziri wa Mambo ya Nje kimetoa taarifa kikisema kwamba kufanyika kikao hicho katika eneo lililotajwa ni kinyume na maazimio ya kimataifa yanayolitambua eneo la Quds Tukufu kuwa eneo linalokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imesema kwamba kufanyika kikao cha kimataifa katika Quds Tukufu ni hatua hatari ambayo inapaswa kusimamishwa mara moja.
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Kiarabu wamelitaka shirika la WHO kusimamisha mara moja kikao hicho ili kuchangia juhudi za kimataifa za kufikiwa amani na utulivu wa kudumu katika ardhi za Palestina na hasa katika eneo la Quds Tukufu.
Kabla ya hapo Jumuiya ya Nci za Kiarabu ilimtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na viongozi wa nchi za Ulaya kuingilia kati na kusimamisha kikao hicho huko Quds na kukihamishia sehemu nyigine. 905389
captcha