Hamad bin Sheikh Ahmad al Shaibani ametoa amri ya kuundwa kamati hiyo.
Wakati huo huo Abdur Rahim Muhammad Tahir Naibu Mwenyekiti wa mpango wa kuchapisha na kusambaza msahafu wa kitaifa wa Imarati amesema kuwa kuundwa kamati hiyo ni hatua muhimu katika njia ya kuchapisha msahafu wa kitaifa ambayo matunda yake yanaonekana siku baada ya siku.
Ameongeza kuwa kamati hiyo inafanya mashauriano na wataalamu na wakosoaji kwa ajili ya kuunda kundi la kusimamia uchapishaji wa msahafu huo. 906395