Programu hiyo imetayarishwa na Baraza la Uhusiano wa Kiislamu na Marekani (CAIR) kama jibu na kejeli iliyofanywa na mtu aliyejulikana kwa jina la Kamal Saliim dhidi ya Uislamu.
Mtu huyo ambaye kwa sasa ni Mkristo anatumia fursa yoyote anayopata kwa ajili ya kuuhujumu Uislamu.
Hivi karibuni Mmarekani huyo aliuhujumu Uislamu na Waislamu katika shughuli ya dua iliyofanyika Kansas City.
Baada ya mkasa huo Baraza la Uhusiano wa Kiislamu na Marekani lilichukua uamuzi wa kutayarisha ratiba hiyo ya kuwatambulisha watu mafundisho ya dini ya Kiislamu na Mtume Muhammad (saw). 905634