Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Amana Bank, Haroon Pirmohamed aliwaambia waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi kuwa benki hiyo itawawezesha wafanyabiashara na makundi mbalimbali ya dini hiyo kufanya shughuli zao za kifedha bila kuathiri misingi ya imani yao.
Alifafanua kuwa pamoja na huduma zitakazotolewa na benki hiyo kufuata misingi ya dini ya Kiislamu, zitawahusu pia watu wa makundi yote wakiwamo wa dini nyingine wanaoamini mfumo wa kibenki unaofuata sheria za Kiislamu.
Alitaja moja ya misingi iliyomo katika mfumo wa sheria za Kiislamu kuwa ni kuendesha benki isiyotoza riba.
Parimohamed alizitaja huduma zitakazotolewa na benki hiyo kuwa ni kama akaunti za akiba, akaunti ya watoto, wanawake na Hija. Amana Bank ndio benki ya kwanza kamili ya Kiislamu nchini Tanzania. Katika nchi jirani ya Kenya tayari kuna banki mbili za Kiislamu.
906702