Kiongozi wa kundi hilo Ismail Rahdar amesema kwamba Qur'ani hiyo muhimu na yenye thamani kubwa itawekwa kwenye jumba la maonyesho la Imam Hussein (as) ili waumini wanaofanya ziara katika sehemu hiyo takatifu wapate fursa ya kuiona.
Qur'ani hiyo imeandikwa kwa mkono kwa ushirikiano wa wasanii ambao wanajumuisha waandishi, wakufunzi, walimu na madaktari wenye shauku na mapenzi makubwa kwa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw).
Rahdar amesema kuwa nuskha hiyo ya Qur'ani iliyo na kurasa 610 ilianza kuandikwa kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Ja'far Swadiq (as) na kukalimika kwa mnasaba wa kuzaliwa Imam Ali bin MUssa Ridha (as), ambapo karibu wanakaligrafia 1000 walishirikiana kuiandika.
Wakati huohuo Abdul Mahdi Karbalai, Msimamizi wa Haram ya Imam Hussein (as) amesifu na kupongeza hatua hiyo ya wasanii wa Iran. 906745