Tuzo hiyo ya kimataifa imekabidhiwa na Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Uislamu Abdullah bin Abdul Muhsin al Turki katika sherehe zilizofanyika mjini Jiddah Saudi Arabia.
Jumuiya ya Kulinda Qur'ani ya Jordan imetunukiwa tuzo hiyo kutokana na kuwa na sifa kama kuwa na aina mbalimbali za shughuli za Qur'ani, nidhamu nzuri ya uendeshaji wa masuala ya kiidara, taathira kubwa za jumuiya hiyo, kutumia vyema suhula mbalimbali na kadhalika.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa Tuzo ya Kimataifa ya Kuhudumia Qur'ani Tukufu ilianzishwa mwaka 1426 Hijria kwa lengo la kuenzi vituo, taasisi na walimu hodari wa Qur'ani kwa shabaha ya kuzidisha motisha na moyo wa ushindani kati ya vituo vya elimu na mafunzo ya Qur'ani. 906980