Gazeti la Daily Mail la Uingereza limeandika kuwa wanachuo hao waliamua kuondoka darasani kutokana na nadharia hiyo ya Darwin kupingana na mafundisho ya Qur'ani kuhusu maumbile ya dunia.
Wahadhari wa chuo hicho wamekuwa wakilalamikia suala la kuondoka darasani wanafunzi kutokana na kupinga nadharia za Darwin.
Mhadhiri Richard Dowkins wa Chuo Kikuu cha Oxford amesema kuwa idadi ya wanafunzi wanaoondoka darasani kutokana na kupinga nadharia za Charles Darwin inaongezeka siku baada ya siku.
Amesema aghlabu ya wanafunzi hao ni Waislamu ambao wanafuatwa na wanafunzi wa dini nyinginezo.
Kwa mujibu wa nadharia hiyo ni kuwa viumbe vimepatikana hatua kwa hatua kupitia mabadiliko hadi kufikia mauimbile yao ya sasa.906482