Ubalozi huo umesema kuwa Balozi Ghadhamfar Rukn Abadi, anayewakilisha Jamhuri ya Kiislamu nchini Lebanon amekutana na kuzungumza na baadhi ya shakhsia wa kisiasa, kijamii, kiutamaduni na wasomi pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu nchini Lebanon kuhusiana na njia za kufanikisha kikao hicho cha Afrika Kusini.
Taarifa iliyotolewa na ubalozi huo imesema kuwa watu aliokutana nao Balozi Rukn Abadi ni pamoja na wanaharakati walioshiriki hivi karibuni katika msafara wa meli za kuvunja mzingiro wa kidhulma unaotekelezwa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza. Wanaharakati hao wanatoka katika nchi za Misri, Marekani, Saudi Arabia, Jordan, Algeria, Sudan, Morocco, India, Yemen, Tunisia, Syria, Palaetsina, Afrika Kusini, Lebanon, Uingereza, Uholanzi na Hispania.
Balozi Rukn Abadi amewashukuru wanaharakati hao kutokana na juhudi zao za kufichua na kuvunja njama zinazotekelezwa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia kwa ushirikiano wa serikali ya Marekani.
Balozi Rukn Abadi amesema kuwa kuyagonganisha makundi ya kidini na kimadhehebu ni mbinu hatari zaidi inayotumiwa na Marekani na utawala wa Kizayuni katika kuvuruga umoja wa mataifa tofauti. 907676