IQNA

Vikwazo vyazidishwa dhidi ya shule za Kiislamu nchini Uingereza

12:24 - November 30, 2011
Habari ID: 2231845
Licha ya kuongezeka idadi ya Waislamu wanaotaka kunufaika na masomo katika shule za Kiislamu nchini Uingereza, lakini vikwazo na siasa za mibano zimekuwa zikiongezeka kila siku dhidi ya juhudi za Waislamu za kuasisi shule mpya ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi wanaotaka kujiunga na shule hizo.
Kwa mujibu wa tovuti ya onislam.net shule za Kiislamu nchini Uingereza zinaendelea kubanwa na sheria za kidhulma na uonevu dhidi ya Uislamu. Wakuu wa elimu wa Uingereza wanadai kwamba wanatekeleza sheria hizo kali dhidi ya Waislamu kwa lengo la kulinda viwango vinavyokubalika vya masomo. Lakini wakuu wa shule za Kiislamu wanasema kuwa huo ni uongo mtupu usiokuwa na msingi kwa sababu hamu waliyonayo wanafunzi wa Kiislamu wanaotaka kujiunga na shule hizo ni thibitisho tosha kwamba shule hizo zinazingatia vyema viwango vya masomo vinavyokubalika na Wizara ya Elimu ya Uingereza.
Kuna shule za Kiislamu zipatazo 140 nchini Uingereza ambapo 60 kati ya hizo zilifunguliwa katika miaka 10 iliyopita. Waislamu wanaoishi Uingereza wanakadiriwa kuwa milioni 2.5. 908262
captcha