IQNA

Kikao cha OIC kuhusu Syria chafanyika Jeddah

12:36 - December 01, 2011
Habari ID: 2232377
Kikao cha dharura cha Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC kimefanyika katika makao makuu ya jumuiya hiyo huko Jeddah Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa Gazeti la al-Yaum as Sabe' linalochapishwa nchini Misri, kikao hicho kimehudhuriwa na Walid Muallim, Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria na Ali Akbar Swalehi waziri mwenzake wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran miongoni mwa shakhsia wengine muhimu wa nchi wanachama. Wawakilishi wa nchi zote 57 wanachama walialikwa kushiriki katika kikao hicho kilichofanyika hapo jana Jumatano.
Kabla ya kuanza kikao hicho, Profesa Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa OIC alitahadharisha dhidi ya kuchochewa mgogoro wa Syria na kufanywa kuwa wa kimataifa. Ametahadharisha dhidi ya njama zinazofanywa na baadhi ya madola ya Magharibi za kuingilia masuala ya ndani ya Syria na kuonya kwamba jambo hilo linaweza kuhatarisha usalama, amani na uthabiti wa eneo zima la Mashariki ya Kati. 908478
captcha