Chama cha Uhuru na Uadilifu cha Ikwanul Muslimin kinaongoza katika matokeo ya awali ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge.
Mjini Cairo wafuasi wa Ikwanul Muslimin wamepata asilimia 47 ya kura zilizopigwa. Uchaguzi wa Baraza la Chini la Bunge la Misri utaendelea katika duru tatu kwa muda wa wiki sita.
Kuna wapiga kura milioni 40 nchini Misri na uchaguzi huu unatathminiwa kuwa hatua ya kwanza ya kuwaondoa madarakani watawala wa kijeshi na kuiweka madarakani serikali ya wananachi.
Uchaguzi huu ndio wa kwanza tokea mwamko wa Kiislamu wa wananchi umuangushe dikteta Husni Mubarak mwezi Februari. Harakati ya Ikwanul Muslimin ilipigwa marufuku wakati wa utawala wa Mubarak.908767