IQNA

Wikipedia ya Kiislamu kuanzishwa

13:56 - December 03, 2011
Habari ID: 2232817
Mkurugenzi wa mradi wa kuanzisha mtandao wa kwanza wa kijamii wa Kiislamu amesema Wikipedia ya Kiislamu itaanzishwa kama sehemu ya mradi huo.
Ahmad Azimov amesema mjumuiko wa vitabu vya Kiislamu na marejeo yanatayarishwa ili kuzindua Wikipedia ya Kiislamu, imeripoti tovuti ya lepost.
Ameashiria juhudi za kuanzisha mtandao huo wa kijamii wa Kiislamu ujulikanao kwa jina la ‘Salam World’ na kusema lengo lake ni kuwavutia watumiaji milioni 50 katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
‘Katika mtandao wa jamii wa Kiislamu, maadili na mafundisho ya Kiislamu yatajadiliwa’, amesema Azimov na kusisitiza kuwa mijadala yoyote iliyodhidi ya Uislamu haitoruhusiwa.
Ameongeza kuwa mtandao hu utakuwa na makao yako huko Istanbul, Uturuki na matawi 30 katika miji kama vile Cairo, Moscow na New York.
Azimov ameendelea kusema kuwa mtandao wa Salam World utakuwa na lugha 15.
909402
captcha