IQNA

Hizbullah yalaani vikwazo vya Wamagharibi dhidi ya Iran

14:08 - December 03, 2011
Habari ID: 2233218
Harakati ya Mapambano ya Lebanon, Hizbullah imelaani vikwazo vya hivi karibuni vya madola ya kimagharibi dhidi ya Iran na kuvitaja kuwa ni vya kichokozi na kidhalimu.
"VIkwazo hivi ni sehemu ya kampeni ya kimataifa dhidi ya Iran, Syria, watu wa eneo la Mashariki ya Kati na mrengo wa muqawama na mapambano ambao unapinga sera hasimu za Wamagharibi kwa miongo kadhaa", imesema taarifa ya Hizbullah.
"Hizbullah inalaani vikali maamuzi haya ya kichokozi na yasiyo na uadilifu na inatoa wito wa ushirikiano zaidi wa kiuchumi baina ya nchi zinazolengwa na vikwazo vya nchi za Magharibi ili kuvunja njama hizi'.
Marekani na waitifaki wake wa Kimagharibi wametangaza vikwazo vipya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika sekta za benki, viwanda vya petrokemikali, mafuta na gesi kwa lengo eti la kuitenga Iran.
Marekani na waitifaki wake wa Kimagharibi hasa Uingereza na Ufaransa wamechukua hatua ya pupa ya kuongoza vikwazo vipya dhidi ya Iran wakati walipopoteza matumaini ya kupitisha azimio kali dhidi ya Iran katika Bodi ya Magavana ya IAEA na kupeleka tena faili la Iran katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Duru za kidiplomasia zinasema kuwa kutekelezwa vikwazo dhidi ya Iran katika wakati ambao Marekani na nchi za Ulaya zinakabiliwa na matatizo chungu nzima ya kiuchumi kutakuwa jambo gumu sana. Ni kwa sababu hii ndio maana baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya kama vile Ujerumani, zinaamini kuwa kuiwekea Iran vikwazo kutayatia hasara mashirika ya Ulaya kwani nafasi yao nchini Iran itachukuliwa na mashirika ya Russia, China na nchi zingine za Asia.
Nukta nyingine ni kuwa vikwazo vya Wamagharibi vimelifanya taifa la Iran kuwa bunifu na hatimaye kujitosheleza katika sekta mbalimbali.

909692
captcha