Nakala hiyo ya Qur'ani ambayo imepambwa kwa maji ya zafarani na wino wa Kichina, iliandikwa miaka 300 iliyopita na iliwavutua watazamani wengi katika maonyesho ya kimataifa ya mapambo ya nyumbani yaliyomaliza kazi zake jana mjini Jeddah.
Msimamizi wa maonyesho hayo Najlaa Falmban amesema kuwa bidhaa zilizoonyeshwa kwenye maonyesho hayo zimevutia watazamaji wengi lakini nakala hiyo ya Qur'ani ya kale ndio iliyotia fora kwa kuvutia idadi kubwa zaidi. 909406