IQNA

Wasomaji bora wa Qur'ani kuenziwa Senegal

17:59 - December 03, 2011
Habari ID: 2233515
Sherehe za kuwaenzi washindi wa mashindano ya kiraa ya Qur'ani makhsusi kwa ajili ya watoto itafanyika tarehe 6 Disemba katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.
Kituo cha habari cha APS kimeripoti kuwa sherehe hiyo itafanyika nyakati za asubuhi chini ya usimamizi wa Harakati ya Mshikamano na Udugu wa Kiislamu ya Senegal (MFSI) katika Msikiti wa Madina mjini Dakar.
Watoto waliofanya vizuri katika mashindano hayo ya Qur'ani watatunukiwa zawadi na baadaye kutafanyika vikao vya dua na kiraa ya Qur'ani Tukufu.
Vilevile kutafanyika mchango wa fedha kwa ajili ya kuboresha hali ya shule na madrasa za Qur'ani na familia zisizojiweza. 909894
captcha