Gazeti la al Sharq limeripoti kuwa awamu ya kwanza ya duru ya sita ya mashindano ya kitaifa ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani ya Sheikh Ghanim upande wa wanaume ilianza Alkhamisi iliyopita ikiwashirikisha wanafunzi wa kiume wa vyuo vikuu, na yale ya wanawake yanatazamiwa kuanza leo Jumapili tarehe 4 Disemba. Mashindano hayo yataendelea hadi Alkhamisi ijayo.
Mashindano hayo ya Qur'ani yanafanyika katika vitengo 11 ikiwa ni pamoja na kuhifadhi Qur'ani nzima na tajwidi, usoma mzuri na tafsiri ya misamiati ya juzuu ya 30 ya Qur'ani, hifdhi ya juzuu 25 na tajwidi na usomaji mzuri na tafsiri ya sura za kuanzia A'laa hadi suratun Nas na kuhifadhi juzuu 20 na tajwidi, usomaji mzuri na tafsiri ya misamiati ya Qur'ani ya sura za kuanzia Adh'dhuha hadi suratun Nas.
Katika upande wa kiraa kutakuwepo mashindano ya udhibiti wa kiraa kamili ya Qur'ani na kulinda sheria za tajwidi makhususi kwa watoto wenye umri wa miaka 15, kiraa ya nusu ya Qur'ani kwa watoto wenye umri wa miaka 9 hadi 14 na kiraa ya juzuu ya Amma makhsusi kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 8.
Washiriki katika mashindano hayo wataenziwa na kupewa zawadi. 909892