IQNA

OIC yalaani mpango wa Israel kujenga vitongoji zaidi

11:48 - December 04, 2011
Habari ID: 2233914
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC, Proofesa Ekmeleddin Ihsanoglu amelaani vikali hatua ya utawala haramu wa Israel kuidhinisha ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kizayuni huko Quds Tukufu (Jerusalem).
Ihsanoglu katika taarifa aliyoitia Jumamosi amesema mpango huu mpya wa Wazayuni unalenga kuutenganisha mji wa Quds na maeneo mengine ya Wapalestina na hivyo kubadilisha muundo wa kidemografia jambo ambalo linakiuka kabisa sheria za kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa.
Aidha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa Kamati ya Pande Nne (Quartet) na Baraza la Umoja wa Mataifa kutekeleza majukumu yao na kuchukua msimamo unaofaa kuzuia vitendo vya kichokozi vya utawala wa Kizayuni katika kipindi hiki nyeti. Aidha ametaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya utawala wa Kizayuni ili usitishe sera zake za kughusubu ardhi za Palestina hasa Quds Mashariki sana.
910609
captcha