IQNA

Iran kuimarisha shughuli za Qur’ani duniani

15:11 - December 04, 2011
Habari ID: 2233946
Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu la Iran (ICRO) limetangaza kuwa kuimarisha shughuli za Qur’ani ni kati ya mambo ambayo yanapewa umuhimu katika vituo vya utamaduni vya Iran kote duniani.
Ahmad Zarnegar Mkuu wa Masuala ya Qur’ani ya shirika la ICRO amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa kuna mipango mipya ya shughuli za Qur’ani katika vituo vya utamaduni vya Iran duniani.
“Tumevitaka vituo vyetu vyote kutangaza mipango yao ya kuimarisha shughuli za Qur’ani”, amesema na kuongeza kuwa kila nchi ina masharti na mazingira tafauti na hivyo mipango ya kuimarisha shughuli za Qur’ani inatafautiana kutoka nchi hadi nyingine.
Amesema kuna mipango ya kuandaa wiki za Qur’ani katika miezi mingine mbali na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Zarnegar amesema kutakua na wiki za Qur’ani katika siku za Alfajiri Kumi, mwezi Februari, ambapo huadhimishwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na vilevile kwa mnasaba wa Maulidi ya Mtume SAW.
909756
captcha