Amesema hatua ya bunge kupunguza uhusiano na Uingereza ni zawadi kwa taifa la Iran.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ameongeza kuwa, vikosi vya kijeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vimejiandaa na vitatoa jibu kali kwa uvamizi wowote ule dhidi ya ardhi ya nchi hii.
Sheikh Siddiquie amewaonya maadui kwa kuwaambia kwamba, Iran haitishiki na kitisho chochote kile na kwamba, vikosi vya kijeshi vya Iran viko macho na vimejiandaa kujibu chokochoko yoyote ile ya kijeshi kutoka kwa adui.
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ameashiria hatua ya jeshi la Iran ya kuangushwa ndege ya kisasa kabisa ya Marekani isiyo na rubani baada ya kuingia katika eneo la mashariki mwa nchi mapema wiki hii na kubainisha kwamba, hatua hiyo inaonyesha uwezo mkubwa wa jeshi la Iran.
Maafisa wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Jumapili walitangaza kuwa kitengo cha ulinzi wa anga na vita vya kielektroniki katika Jeshi la Iran lilifanikiwa kudhibiti hali ya anga na upashaji taarifa na kuweza kuiangusha kitaalamu ndege ya kijasusi isiyo na rubani ya Marekani aina ya RQ-170 Sentinel. Marekani imekiri kuwa ndege hiyo iliyotokea katika kituo chake huko Afghanistan ilikuwa ikitumiwa na Shirika la Ujasusi la Marekani CIA kufanya ujasusi nchini Iran.
912251