Mashindano hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu, Zawadi ya Dubai. Ibrahim Muhammad Bu Mulihha, mkuu wa kamati iliyosimamia mashindano hayo anasema kuwa zawadi nono na za thamani kubwa zilitolewa kwa mahafidhi wote 12 walioshiriki kwenye mashindano hayo.
Duru ya nane ya mashindano ya al-Hafith al-Muwatin ilianza mjini Dubai siku ya Jumamosi Novemba 26 kwa kuwashirikisha washindani 12 wa kike na kiume kutoka nchini Imarati.
Taasisi ya Kimataifa ya Qur'ani, Zawadi ya Dubai pia inajitayarisha kuandaa duru ya 13 ya mashindano ya kitaifa ya Qur'ani na tarehe ya kuanza kusajiliwa majina ya washiriki wa mashindano hayo itatangazwa hivi karibuni. 912212