Akifafanua suala hilo katika maombolezo ya Shahid Imam Hussein (as) yaliyofanyika siku ya Alkhamisi tarehe 8 Disemba Pir Muhammad Naqib ar-Rahman amesema kuwa Imam Hussein (as) alifanya mapambano na kuuawa shahidi kwa ajili ya kuhuisha utukufu wa Uislamu na kutekeleza sheria za Mwenyezi Mungu na kuwataka Waislamu wadumishe njia yake hiyo tukufu. Amesema kuwa kujitolea kwa Imam Hussein (as) na wafuasi wake wachache katika tukio la Karbala ni jambo lisilokuwa na mfano wake katika historia nzima ya mwanadamu.
Pir Muhammad ameongeza kuwa wafuasi wa Imam Hussein (as) walishinda mtihani wa Mwenyezi Mungu na kupata utukufu wa milele kwa kuweka kando matamanio yao ya kidunia.
Amesisitiza juu ya kuimarishwa umoja miongoni mwa Waislamu na kusema kuwa Waislamu duniani wanaweza kushinda changamoto zote zinazowakabili kupitia umoja na mshikamano.
Idadi kubwa ya maulamaa, wasomi na wanafikra wa Kiislamu kutoka mji wa Rawalpindi na miji mingine ya Pakistan walishiriki katika maombolezo hayo yaliyofanyika katika Haram ya Idgah. 912220