IQNA

Sehemu ya ibada yajengwa katika Chuo Kikuu cha Munouba nchini Tunisia

15:18 - December 11, 2011
Habari ID: 2236495
Mkuu wa Kitengo cha Fasihi na Elimu za Kijamii katika Chuo Kiku cha Manouba nchini Tunisia amesema kuwa kwa mara ya kwanza msikiti utajengwa kwenye chuo hicho kwa ajili ya kutoa nafasi ya kufanyika ibada na swala za jamaa katika mazingira ya chuo hicho.
Kwa mujibu wa tovuti ya businessnews, kwa mara ya kwanza katika historia ya Tunisia, wanachuo wa chuo hicho wamekuwa wakitekeleza ibada na swala za jamaa katika maeneo ya wazi ya chuo hicho kufuatia kung'olewa madarakani kwa utawala wa dikteta Bin Ali na kuingia madarakani kwa chama cha Kiislamu cha an-Nahdha.
Kabla ya kutolewa tangazo la kujengwa msikiti huo, wanachuo wa chuo hicho wamekuwa wakifanya mgomo wakitaka kutolewa kibali cha kujengwa msikiti katika uwanja wa chuo hicho.
Habib Kozdoghli, mkuu wa Chuo cha Manouba akizungumza na vyombo vya habari vya Tunisia amesema kuwa uongozi wa chuo hicho wamechukua uamuzi wa kujenga msikiti huo baada ya wanachuo kutoa mashinikizo ya kutaka kujengwa msikiti ili kusimamisha swala za jamaa.
Amesema pia kwamba wanachuo wa kike wanaweza kuhudhuria masomo katika chuo hicho wakiwa wamevalia vazi la stara kwa mwanamke wa Kiislamu, yaani hijabu. 913298
captcha